Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imefanya Makabidhiano ya Eneo la Ujenzi wa Dahalia na Kampuni ya Ujenzi United Rump katika Chuo cha Kiislam Pemba .
Katika makabidhiano hayo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh.Lela Mohd Mussa amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya United Rump kuharakisha Ujenzi wa Dahalia katika Chuo hicho ili Wanafunzi waweze kuondokana na Usumbufu wanaoupata .
Akipokea eneo la Ujenzi wa Dahalia hio Meneja wa Mradi kutoka Kampuni ya United Rump Mhandisi Said Salim Hamad ameahidi kufanya kazi hio kwa weledi na kwa muda waliokubaliana, sambamba na Kujenga Eneo la Chakula kutokana na faida wanaotarajia kuipata katika Ujenzi huo.
Nae Mhandisi kutoka Wizara ya Elimu Eng. Khamis Mtara aeleza namna ya Ujenzi wa Dahalia hio utakavyokua.