Serikali italipa fidia Wananchi vipando vyao vimeathiriwa kwa kupisha Ujenzi wa Nyumba za Gharama nafuu katika Eneo la Chumbuni.
Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe. Salha Mwinjuma amesema inaendelea na kutathamini katika Eneo hilo na Wananchi wote watalipwa fidia zao kulingana na miongozo na kanuni ziliopo.
Katika Kikao hicho cha pamoja baina ya Uongozi wa Wizara,Viongozi wa Mkoa, Jimbo na Wananchi huko Chumbuni Mhe, Salha amesema kuwa mpango huo utafanyika mara baada ya tathmini.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa ameipongeza Serikali kwa kuleta Mageuzi na Mapinduzi katika Sekta ya Makaazi kwa kuhakikisha kuwa na Makaazi bora na salama kwa Wananchi wake.
Akitoa ufafanuzi Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba Zanzibar Sultan Said Suleiman amefahamisha kuwa Ujenzi huo unatarajiwa kujengwa kwa Awamu Tatu na utajumisha Nyumba Elfu Tatu 3000 ambapo kwa hatua ya Awali Nyumba zaidi ya Elfu Moja zitajengwa na hakuna Nyumba ya Mwananchi itakayoathirika na Ujenzi huo.
Nao Wananchi wamepongeza kwa kuchagua Eneo la Chumbuni kuweza kujenga Nyumba za Kisasa ambazo zitaleta haiba na wameahidi kutoa ushrikiano.
Ujenzi wa Nyumba za Gharama Nafuu Elfu Tatu ambazo zitajengwa katika Eneo la Chumbuni na Kampuni ya Weihai ya China utajumuisha huduma muhimu zikiwemo Skuli na Hospital.