Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ina fursa nyingi za Uwekezaji hivyo amewataka Wawekezaji kutoka Marekani wazitumie fursa hizo kwa kuekeza Zanzibar.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo huko Ikulu wakati alipotembelewa na Wabunge wa Bunge la Senate la Marekani, amesema Serikali imeipa kipaumbele Sekta ya Uchumi wa Buluu kwani ni moja ya Eneo linatoa fursa nyingi za Ajira kwa Jamii
Amewaeleza Wabunge hao kuwa Zanzibar ina mipango Mikakati ya kuimarisha Sekta ya Viwanda ili kupunguza gharama ya uagizaji bidhaa kutoka Nje ya Nchi, pia kutoa nafasi kusafirisha bidhaa za Zanzibar Nje ya Nchi.
Aidha Dkt. Mwinyi ametoa ufafanuzi kuhusu Serikali inavyopambana na ukosefu wa Ajira kwa kutoa Elimu ya vitendo kwa Vijana ikiwa na lengo la kuwaandaa kuweza kujiajiri Wenyewe.
Katika maelezo yake Dkt. Mwinyi amesema ujio wa Wageni hao utatoa nafasi ya kuendeleza Mashirikiano yaliopo baina ya Nchi Mbili hizo.