WAMILIKI WA HOTELI WATAKIWA KUSIMAMIA MAZINGIRA YA USAFI WA FUKWE

Meneja wa hifadhi ya Kisiwa cha Mnemba na huba ya Chwaka Ndg.Omar Hakim Foum amewasihi wamiliki wa hoteli za kitalii kushirikiana kufanya usafi maeneo ya Fukwe za Zanzibar ili kuweka haiba nzuri za fukwe na kuendelea kuwavutia Watalii.

Akizungumza baada ya kufanya usafi wa mazingira uliowashorikisha Wafanya kazi wa Hoteli huko Nungwi amesema lengo la kufanya usafi Eneo hilo ni kuona maeneo ya Fukwe yanakuwa safi ili kuendana na dhamira ya Uchumi wa Buluu.

UPATIKANAJI BIDHAA ZA FUTARI WARIDHISHA KATIKA SOKO LA MAJENGO

Wafanya Biashara wa bidhaa za Vyakula na Viungo katika Soko la Majengo Jijini Dodoma wamesema upatikanaji wa bidhaa hizo umekuwa wa kuridhisha hali inayoleta taswira nzuri ya upatikanaji wa Futari katika Kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wakizungumza na ZBC wamesema bidhaa nyingi tayari zimeshafikishwa Sokoni hapo ikiwemo Ndizi, Mihongo, Viazi Vitamu, Mbatata na Maharage kwa ajili ya maandalizi ya Mwezi huo.

Subscribe to
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.