DKT.MWINYI AITAKA JAMII KUHAKIKISHA WANASIMAMIA VYEMA MAADILI KWA WATOTO NA VIJANA

DKT.MWINYI

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amehimiza Malezi bora katika Jamii na kuhakikisha wanasimamia  vyema  maadili kwa Watoto na  Vijana ili kunusuru Taifa.

     Dkt. Mwinyi amesema hayo wakati  akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya Ibada ya Sala ya Ijumaa

iliyofanyika Masjid Taqwa  Mwanakwerekwe Meli Nne Wilaya ya Magharibi 'b' Mkoa wa Mjini Magharibi.

     Amesema  ni wajibu wa kila Mmoja kuhakikisha anasimamia Malezi ya Watoto na Vijana kutokana  na kuwa wakati  umebadilika na  utandawazi na Vijana hujifunza mengi kupitia Mitandao ya kijamii.   

   Rais Dkt. Mwinyi amehimiza kuendelea kuliombea Taifa na  kudumisha amani,utulivu, umoja na mshikamano ili kuzidi  kupiga

hatua ya maendeleo.

    Katibu Mtendaji Ofisi ya  Mufti  wa Zanzibar Shekhe Khalid Ali Mfaume amewataka Waumini na Jamii kuendelea kumuombea Dua Mhe. Rais kuendelea kutekeleza mipango ya Maendeleo

     Awalii  Khatib wa Sala hiyo Shekhe Khatib Omar Khatib amewahimiza Waislamu kuongeza juhudi  katika kutumia akili na maarifa katika kufuata maagizo ya Mwenyezi Mungu ili kupata Mafanikio huko Akhera.                       

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.