Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amehimiza Malezi bora katika Jamii na kuhakikisha wanasimamia vyema maadili kwa Watoto na Vijana ili kunusuru Taifa.
Dkt. Mwinyi amesema hayo wakati akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya Ibada ya Sala ya Ijumaa
iliyofanyika Masjid Taqwa Mwanakwerekwe Meli Nne Wilaya ya Magharibi 'b' Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema ni wajibu wa kila Mmoja kuhakikisha anasimamia Malezi ya Watoto na Vijana kutokana na kuwa wakati umebadilika na utandawazi na Vijana hujifunza mengi kupitia Mitandao ya kijamii.
Rais Dkt. Mwinyi amehimiza kuendelea kuliombea Taifa na kudumisha amani,utulivu, umoja na mshikamano ili kuzidi kupiga
hatua ya maendeleo.
Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti wa Zanzibar Shekhe Khalid Ali Mfaume amewataka Waumini na Jamii kuendelea kumuombea Dua Mhe. Rais kuendelea kutekeleza mipango ya Maendeleo.
Awalii Khatib wa Sala hiyo Shekhe Khatib Omar Khatib amewahimiza Waislamu kuongeza juhudi katika kutumia akili na maarifa katika kufuata maagizo ya Mwenyezi Mungu ili kupata Mafanikio huko Akhera.