WAMILIKI WA HOTELI WATAKIWA KUSIMAMIA MAZINGIRA YA USAFI WA FUKWE

USAFI FUKWE
English

Meneja wa hifadhi ya Kisiwa cha Mnemba na huba ya Chwaka Ndg.Omar Hakim Foum amewasihi wamiliki wa hoteli za kitalii kushirikiana kufanya usafi maeneo ya Fukwe za Zanzibar ili kuweka haiba nzuri za fukwe na kuendelea kuwavutia Watalii.

Akizungumza baada ya kufanya usafi wa mazingira uliowashorikisha Wafanya kazi wa Hoteli huko Nungwi amesema lengo la kufanya usafi Eneo hilo ni kuona maeneo ya Fukwe yanakuwa safi ili kuendana na dhamira ya Uchumi wa Buluu.

Amesema Sekta ya Utalii Zanzibar ni Sekta Mama ya kiuchumi hivyo ni vyema kwa Hoteli za kitalii kuweka mazingira za safi ya fukwe ambazo ni kivutio cha Watalii wanaofika Zanzibar.

Afisa uhifadhi rasilimali za bahari Zanzibar Ali Rashid Amour amesema mazingira ni moja ya mkakati wa Utalii Zanzibar hivyo amewataka Wananchi na Watumiaji wa Bahari kuhifadhi taka za plastiki ili  kulinda maisha ya Viumbe Hai wa bahari.

Nao Wasimamizi wakuu na Wafanya kazi wa Hoteli za Mkoa wa Kaskazini Unguja, wamesema kazi hiyo ya Usafi haitaishia hapo bali itakuwa endelevu kwa ustawi wa Sekta ya Utalii.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.