MHE. AYOUB APIGA HATUA KUBWA KUTEKELEZA AHADI KWA VITENDO
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Chaani, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, ameendelea kuimarisha uhai wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kukamilisha ukarabati wa matawi mawili kwa kupiga plaster, huku tawi la Ketwa likiwa hatua za mwisho.
Mhe. Ayoub alizungumza hayo katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika visiwani Zanzibar, ambapo alibainisha kutenga shilingi milioni 20 kwa ajili ya mashindano ya Qur'an ya jimbo ili kuimarisha umoja wa wananchi wa Chaani.



