DKT.MWIGULU ATOA WIKI MBILI KWA WIZARA YA MAJI KUTAFUTA MKANDARASI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba ameipa Wizara ya Maji Wiki mbili kuhakikisha inakamilisha utaratibu wa upatikanaji wa Mkandarasi wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka chanzo cha Ziwa Chala.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Marangu-Kitowo, Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro baada ya kupokea taarifa za Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka chanzo cha Ziwa Chala, Ujenzi wa Mradi wa Barabara holili(Rotima)-tarakea(nayemi), pamoja kuweka jiwe la msingi la skuli ya sekondari stephen moshi technical. 

SHILINGI BILIONI MOJA ZIMEPATIKANA USAJILI VYOMBO VYA MOTO

Wizara Ya Fedha Na Mipango Imesema Jumla Ya Vyombo Vya Moto Kumi Na Tisa Elfu 337  Vimefanyiwa Usajili Wa Namba Mpya Unaosimamiwa Na Mamlaka Ya Mapato Zanzibar Zra.

Akijibu Suali Katika Kikao Cha Baraza La Wawakilishi Naibu Waziri Wa Fedha Na Mipango Dkt. Hamad Omar Bakari Amesema Kati Ya Vyombo Hivyo Gari Zilikuwa Kumi Na Tatu Elfu Na Sitini Na Kwa Vyombo Nyengine Ni Elfu Sita Mia 277.

Amefahamisha Kuwa Katika Uendeshaji Wa Zoezi Hilo Zaidi Ya Shilingi Bilion Moja Zimekusanywa Kwa Kipindi Cha Miezi Mitatu Tokea Zoezi Hilo Kuanza.

MICHEZO NI FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA

Mbunge Wa Jimbo La Donge Sadifa Juma Khamis, Ameeleza Kuwa Uwepo Wa Viwanja Bora Vya Michezo Ni Muhimu Katika Kukuza Vipaji Sambamba Na Kutoa Fursa Za Ajira Kwa Vijana.

Subscribe to
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.