DKT.MWIGULU ATOA WIKI MBILI KWA WIZARA YA MAJI KUTAFUTA MKANDARASI

DKT.MWIGULU
English

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba ameipa Wizara ya Maji Wiki mbili kuhakikisha inakamilisha utaratibu wa upatikanaji wa Mkandarasi wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka chanzo cha Ziwa Chala.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Marangu-Kitowo, Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro baada ya kupokea taarifa za Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka chanzo cha Ziwa Chala, Ujenzi wa Mradi wa Barabara holili(Rotima)-tarakea(nayemi), pamoja kuweka jiwe la msingi la skuli ya sekondari stephen moshi technical. 

Dkt. Mwigulu amesema Ujenzi wa Mradi huo unapaswa kuanza kutekelezwa kwani unategemewa kutatua changamoto ya upatikanaji wa Maji katika Wilaya nzima ya Rombo.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Wizara haitakuwa kikwazo katika utekelezaji wa Mradi huo na watahakikisha katika Kipindi cha Siku 14 wanampata Mkandarasi wa Mradi huo.

Mradi wa Maji Ziwa Chala unatarajiwa kugharimu Shilingi Bilioni 8.66 na utanufaisha Wananchi 34,104 katika Vijiji 14 vya Wilaya ya Rombo.

Katika hatua nyengine Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Fedha kuhakikisha anatafuta Fedha kwa ajili ya kufanya malipo ya awali kwa Mkandarasi ili aanze ujenzi wa Mradi wa Barabara Holili(Rotima)-Tarakea(Nayemi) Kilomita 52.8

Katika uweka wa Jiwe la msingi la Ujenzi wa Skuli ya Sekondari Stephen Moshi Technical ambayo itagharimu Shilingi Bilioni 1.6 Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema Skuli hiyo ni kielelezo cha uwepo wa Kiongozi mwenye maono na mipango.

 

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.