Wizara Ya Fedha Na Mipango Imesema Jumla Ya Vyombo Vya Moto Kumi Na Tisa Elfu 337 Vimefanyiwa Usajili Wa Namba Mpya Unaosimamiwa Na Mamlaka Ya Mapato Zanzibar Zra.
Akijibu Suali Katika Kikao Cha Baraza La Wawakilishi Naibu Waziri Wa Fedha Na Mipango Dkt. Hamad Omar Bakari Amesema Kati Ya Vyombo Hivyo Gari Zilikuwa Kumi Na Tatu Elfu Na Sitini Na Kwa Vyombo Nyengine Ni Elfu Sita Mia 277.
Amefahamisha Kuwa Katika Uendeshaji Wa Zoezi Hilo Zaidi Ya Shilingi Bilion Moja Zimekusanywa Kwa Kipindi Cha Miezi Mitatu Tokea Zoezi Hilo Kuanza.
Aidha Amesema Katika Uendeshaji Wa Zoezi Hilo Zra Imewekeana Mkataba Na Kampuni Ya Budda Auto Parts Ambao Ndio Wazalishaji Wa Vibati Vya Namba
Dkt. Hamad Amesema Lengo La Kubadilisha Vibati Vya Namba Za Vyombo Vya Usafiri Ni Kutambulikana Kwa Mmiliki Halali Wa Chombo Hicho Na Kuthibiti Uhalifu Unaofanywa Kwa Kutumia Vyombo Hivyo
Wakati Huo Huo Naibu Waziri Wa Uchumi Wa Buluu Na Uvuvi Mhe. Mboja Ramadhan Mshenga Akijibu Suali Katika Kikao Cha Baraza La Wawakilishi Amesema Serikali Inaendelea Kushirikiana Na Kampuni Ya Afrika Geophysical Services Kwa Ajili Ya Kuchukua Taarifa Za Mitetemo Ili Kujua Maeneo Ya Kuchimba Visima Vya Utafutaji Wa Mafuta Na Gesi Asili.
