DKT. MKUYA ATAKA WACHUKULIWE HATUA WAHUDUMU WASIOWASIJIBIKA

Kaimu Waziri Wa Afya Zanzibar Na Waziri Wa Nchi Afisi Ya Raisi Ikulu Dkt Saada Mkuya Salum Amewataka Madaktari Dhamana Ngazi Ya Wilaya Kufanya Kazi Kwa Weledi Ili Sekta Ya Afya Ieandane Na Uwekezaji Uliofanywa Na Serikali.

Akizungumza Katika Mkutano Maalumu Na Viongozi Wa Wizara Ya Afya Pamoja Na Madaktari Hao Dkt. Saada Amesema Kwa Sasa Wananchi Wamekuwa Wakilalamikia Juu Ya Huduma Wanazozipata Katika Vituo Vya Afya Pamoja Na Hospitali, Jambo Ambalo Limekuwa Likiongeza Matatizo Kwa Wagonjwa Wanaofuata Huduma Katika Hospitali Hizo.

WAZIRI MKUU ATAKA JUHUDI ZA UPATIKANAJI MAJI ZIONGEZWE

Waziri Mkuu Wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba Amezindua Teknolojia Mpya Ya Ulipaji Wa Bili Za Maji Kwa Njia Ya Mtandao Na Kuwataka Wakurugenzi Wa Mamlaka Za Maji Safi Na Usafi Wa Mazingira Nchini Kuongeza Juhudi Katika Maeneo Ambayo Bado Wananchi Wanakabiliwa Na Changamoto Ya Upatikanaji Wa Maji.

Dkt. Nchemba Ameyasema Hayo Wakati Akifungua Mkutano Wa Bodi Za Wakurugenzi Wa Mamlaka Za Maji Safi Na Usafi Wa Mazingira Nchini, Mkutano Ulio Lenga Kuwanoa Watendaji Wa Sekta Hiyo Ili Kuongeza Ufanisi Na Uwajibikaji Katika Utekelezaji Wa Miradi Ya Maji.

Subscribe to
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.