Kaimu Waziri Wa Afya Zanzibar Na Waziri Wa Nchi Afisi Ya Raisi Ikulu Dkt Saada Mkuya Salum Amewataka Madaktari Dhamana Ngazi Ya Wilaya Kufanya Kazi Kwa Weledi Ili Sekta Ya Afya Ieandane Na Uwekezaji Uliofanywa Na Serikali.
Akizungumza Katika Mkutano Maalumu Na Viongozi Wa Wizara Ya Afya Pamoja Na Madaktari Hao Dkt. Saada Amesema Kwa Sasa Wananchi Wamekuwa Wakilalamikia Juu Ya Huduma Wanazozipata Katika Vituo Vya Afya Pamoja Na Hospitali, Jambo Ambalo Limekuwa Likiongeza Matatizo Kwa Wagonjwa Wanaofuata Huduma Katika Hospitali Hizo.
Aidha Amesema Kwa Sasa Ni Wakati Wa Madaktari Hao Kuangalia Namna Ya Kusimamia Utolewaji Wa Huduma Kwa Wananchi Kwa Kutumia Rasilimali Zilizopo Pamoja Na Kuwachukulia Hatua Wahudumu Wasiofanya Kazi Zao Inavyotakiwa. Akigusia Suala La Mfuko Wa Bima Ya Afya Zanzibar Dkt Saada Amesema Wizara Ya Afya Inaendelea Kuweka Mikakati Imara Kwa Kushirikiana Na Wizara Ya Fedha Ili Kuona Fedha Zinazopatikana Katika Mfuko Huo Zinarudi Katika Hospitali Na Vituo Vya Afya Kwa Lengo La Kuimarisha Huduma Zinazotolewa.
Kwa Upande Wake, Katibu Mkuu Wizara Ya Afya Zanzibar Dkt. Mngereza Mzee Miraji Ameahidi Kuendelea Kuwasimamia Watendaji Kwa Mujibu Wa Sheria Na Kuona Utendaji Wa Sekta Ya Afya Unaimarika.
Baadhi Ya Changamoto Zilizotajwa Na Madaktari Dhamana Wa Wilaya Ni Pamoja Na Uhaba Wa Watendaji, Usafiri, Vifaa Vya Usafi, Nishati Ya Umeme Pamoja Na Ukosefu Wa Rasilimali Fedha Ambayo Inakwamisha Utendaji Wa Hospitali Na Vituo Hivyo, Wamesema, Licha Ya Malalamiko Yanayotolewa Kwa Uzembe Wa Baadhi Ya Watumishi, Bado Yapo Mengine Ambayo Ni Nje Ya Uwezo Wao.
