SERIKALI KUTUMIA BILIONI 79 KUJENGA VITUO VYA POLISI 698 NCHI NZIMA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema Serikali imepanga kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni 79 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi 698 nchini, ikiwa ni mkakati wa kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

​Akizungumza leo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya Vituo vya Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar Mhe. Ayoub Mahmoud amebainisha kuwa uamuzi huo umekuja baada ya Serikali kuona kuna uhitaji wa kusogeza huduma za Kipolisi karibu na wananchi zaidi.

KIKOSI CHA ZIMAMOTO CHAPOKEA GARI TISA NA BOTI 1

Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar Rashid Mzee Abdallah amesema Kikosi hicho kinaendelea kujiimarisha kwa kuwa na Vifaa vya kisasa vya kukabiliana na Majanga ya Moto.

 

Kamishna Rashid ameyasema hayo baada ya kupokea Gari Tisa za Kuzimia Moto na Boti moja kutoka Nchini Austria.

BILIONI MIA SABA ZATUMIKA KUJENGA KIWANDA CHA SUKARI KILOMBERO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mipango na uwekezaji Professa Kitila Mkumbo amesema kiwanda kipya cha sukari Kilombero K4  kilichopo Mkoani Morogoro ambacho kinajengwa kwa gharama ya shilingi Billioni mia saba kinatarajiwa kuanza uzalishaji wake Mwezi Juni Mwaka huu ni moja ya Kiwanda ambacho kitafanya lengo ya kukuza uchumi kuelekea Mwaka 2050  kufikia dola trilioni moja.

Subscribe to
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.