Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda amepanga kushawishi kutungwa sheria kali itakayowabana wanaopatikana na makosa ya Ubakaji na Ulawiti.
Chatanda ametoa kauli hiyo huko Ukerewe wakati akihutubia Mikutano ya hadhara kwa nyakati tofauti katika Vijiji vya Kagunguli, Nansole na Mjini Nansio.
Amesema kuongezeka kwa vitendo hivyo kunalazimisha kuwepo kwa sheria ambazo zitadhibiti vitendo hivyo viovu.
Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa Mary Pius Chatanda ametembelea Skuli ya Sekondari ya Wasichana Ukerewe, ambako amekagua utekeklezaji wa Miradi Ujenzi wa Mabweni, Madarasa na Vyoo Ujenzi unaogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 900.
Katika hatua nyingine, Chatanda Amezindua Jengo la Biashara na Mradi wa Ushonaji wa UWT Wilaya ya Ukerewe.
Ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, kutoa Elimu ya kupinga ukatili wa Kijinsia, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kuhamasisha Wananchi kushiriki kuimarisha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.