Waziri Mkuu Wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba Amezindua Teknolojia Mpya Ya Ulipaji Wa Bili Za Maji Kwa Njia Ya Mtandao Na Kuwataka Wakurugenzi Wa Mamlaka Za Maji Safi Na Usafi Wa Mazingira Nchini Kuongeza Juhudi Katika Maeneo Ambayo Bado Wananchi Wanakabiliwa Na Changamoto Ya Upatikanaji Wa Maji.
Dkt. Nchemba Ameyasema Hayo Wakati Akifungua Mkutano Wa Bodi Za Wakurugenzi Wa Mamlaka Za Maji Safi Na Usafi Wa Mazingira Nchini, Mkutano Ulio Lenga Kuwanoa Watendaji Wa Sekta Hiyo Ili Kuongeza Ufanisi Na Uwajibikaji Katika Utekelezaji Wa Miradi Ya Maji.
Ametumia Jukwaa Hilo Kuwataka Watanzania Kutunza Na Kuhifadhi Vyanzo Vya Maji Ili Kuendeleza Huduma Hizo Kwa Vizazi Vijavyo.
Kwa Upande Wake, Waziri Wa Maji Jumaa Aweso Ameeleza Kuwa Katika Kipindi Cha Miaka Minne Iliyopita, Serikali Imetekeleza Miradi Ya Maji Ya Zaidi Ya Trilioni Tatu Mjini Na Vijijini, Hatua Inayolenga Kufikia Malengo Ya Dira Ya Taifa Ya Gridi Ya Maji Na Kuhakikisha Wananchi Wengi Zaidi Wanapata Huduma Ya Maji Safi Na Salama.
Nae Katibu Mkuu Wa Wizara Ya Maji Ashura Waziri Ameeleza Manufaa, Ya Mafunzo Yanayo Tolewa Katika Mkutano Huo.
Mbali Na Kufungua Mkutano Huo, Waziri Mkuu Amehitimisha Ziara Yake Jijini Arusha Kwa Kutembelea Ujenzi Wa Stendi Mpya Ya Mabasi Na Kuweka Jiwe La Msingi Katika Soko La Kilombero, Hatua Inayolenga Kuendelea Kuimarisha Miundombinu Na Kuchochea Shughuli Za Kiuchumi Katika Jiji Hilo.
