Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiambatana na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui wakitembelea na kukagua mabanda ya wadhamini pamoja na wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya baada ya kuwasili kwenye Kongamano linalofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaam.
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa anatarajia kufungua rasmi Kongamano hilo la kumbukizi la Rais Mstaafu Mhe. Benjamini Mkapa ambalo limewakutanisha wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya kutoka ndani na nje ya nchi lengo kuu likiwa ni kujadiliana mikakati na changamoto zinazoikabili Sekta ya Afya na namna ya kuzitatua.
stories
standard