Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, Mhe. Ali Suleiman Ameir ameitaka Mamlaka ya Serikali Mtandao kuhakikisha kuwa Serikali inafanikiwa kutumia mifumo ya kieletroniki, kuwa na uwazi katika kutekeleza majukumu ya kila siku na kuhakikisha inatimiza jukumu la kuziunganisha Taasisi mbali mbali za Serikali katika mifumo ya kiserikali.
Mhe. Mrembo ameyasema hayo huko Mazizini wakati wa makabidhiano ya Mamlaka ya Serikali Mtandao Zanzibar iliyokua chini ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala bora, ambayo kwa sasa Mamlaka hiyo imehamishwa na kuwa chini ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar.
Amesema kuwa Mamlaka hiyo ni inaweza kuzalisha vitu vingi ambavyo vitakavyoweza kuleta manufaa na kuwa na tija katika kazi zake na hata ofisi za kiserikali.
Vile vile, amesema ni vyema mifumo yote ya kiserikali isimamiwe vyema na Mamlaka hiyo hususan katika mifumo ya ukusanyaji wa mapato ili kuhakikisha Serikali inafikia lengo la kukusanya mapato bila ya kuwepo kwa upotevu wa fedha za Serikali.