Michezo

TIMU YA JKU IMEONDOKA LEO KUELEKEA KUSHIRIKI MICHUANO YA KAGAME CUP

    Wawakishi  wa Mashindano ya Kombe la Kagame Cup 2024  Zanzibar Timu ya JKU wameondoka Leo  kuelekea Jijini Dar-esaalam kwa ajili ya  Michuano hiyo.

    Kikosi hicho kilicho Jumuisha Wachezaji 25 na Viongozi 7  kimeahidi   kufanya  vizuri  na kuwakilisha vyema zanzibar.

    Katibu Mtendaji Baraza la Michezo Zanzibar  Said Kassim, amesema Zanzibar ina Matarajio makubwa na Timu  ya Jku  kutokana na ubora waliokuwa  nao hivi sasa.

KWEREKWE BINGWA MICHUANO YA FA WILAYA YA MAGHARIBI B

Timu ya Mwanakwerekwe Bingwa Michuano ya FA Wilaya ya Maghari B baada ya kuyadhibu Timu ya Fuoni kwa Bao 1-0 katika Mchezo wa Fainali ya Michuano hiyo.

Michuano hiyo iliyochezwa katika Dimba la Mau ambapo Timu ya  Kwerekwe iliyo Valia Jezi rangi Nyeusi walionesha ufundi wao wa kutafuta goli katika dakika za mapema na hadi  kipenga cha Mwisho cha muamuzi kupigwa Fuoni  ilishindwa kuonesha uhodari wake na kuamuru Ubingwa huo kwenda kwa Kwerekwe.

MICHEZO INA FURSA KUBWA YA KUKUZA IDADI YA AJIRA KWA VIJANA

   Mwenye kiti wa Umoja wa Vijana, CCM Tawi la Magomeni, Shabani Jaffar amesema Michezo ina fursa kubwa ya kupaa Ajira kwaharaka na kutimiza malengo.

   Kauli hiyo ameitoa wakati akikabidhi Mipira ya kuchezea kwa timu ya Azam Zanzibar, huko Uwanja wa Magomeni Mzalendo,ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake kwa Timu hiyo na ameahidi kuendelea kuwaunga mkono Vijana wenizwe kufikia malengo yao.

   Katibu wa Timu ya Azam Zanzibar, Mahmud Juma ameshukurujitihada hizo na amesema tatizo la ukosefu wa Mipira kwa Timu yao lilikua la Muda Mrefu.

JAMII YAKUMBUSHWA KUTUNZA AFYA KWA KUFANYA MAZOEZI

Jamii imekumbushwa kuendelea kufanya Mazowezi na kutunza Mazingira ili kuimarisha afya zao.

Akizungumza mara baada ya Matembezi ya Kilomita Sita na Bonaza la Mazowezi Mlezi wa Barafu Jonging Iddi Azan amesema kufanya Mazowezi ni muhimu kwa Afya na amewataka Vijana kuacha kutumia Vileo ambavyo vinaharibu Maisha yao.

Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara ya Afya Dkt. Ntuli Kapologwe amesema Wizara ya Afya inampango mkakati wa kuimarisha afya ya Jamii kwa kutumia Mabonaza ambayo yanashirikisha Jamii moja kwa moja.

JKU YATWAA UBINGWA WA PBZ PREMIUM LEAGUES

    JKU Sc wamekabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar 'PBZ Premier League' baada ya kumaliza msimu wakiwa na alama 66 juu ya Zimamoto wanaofuata katika nafasi ya pili wakiwa na alama 62.

    JKU wamezawadiwa Kombe, Medali na kitita cha Shilingi Milioni 50.

TIMU YA TAIFA YA KABADDI KUELEKEA KENYA MICHUANO YA KIMATAIFA

   Balozi wa India Nchini Dk. Kumar Praveen amesema ataendelea kuunga mkono Mchezo wa Kabaddi ili uweze kukuwa na kuipeperusha Bendera ya Zanzibar Kimataifa kupitia Mchezo huo wenye asili ya Kihindi. 

    Akizungumza katika Shamra shamra za Siku ya Yoga Kimataifa inayotarajiwa kuadhimishwa June 21 Balozi Kumar amesema Mazoezi na Michezo ni Afya na Ajira hivyo kuunga mkono juhudi za Vijana hao ni kuwasaidia kuwajenga Kiakili, Kiafya na kuwasogeza kufikia ndoto zao.

WAZIRI TABIA AMKABIDHI TUNZO YA HESHIMA MSANII WA TAARAB ASILIA FATMA ISSA

     Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita amesema  kuwepo kwa Tunzo za Wasanii kuna saidia kuleta ari na ushindani katika Tathnia ya Muziki.

    Akizungumza katika Usiku wa Kilele cha Tunzo za Kimataifa za Zanzibar International Music Awards Mh.Tabia amesema hatua hiyo itawawezesha Wasanii kuwapa hadhi na Hamasa ya kufanya kazi ili waweze kuwania Tunzo hizo

TIMU YA MPIRA WA PETE YA BLW KINAJIANDAA NA MASHINDANO MSIMU HUU.

Kikosi cha Timu ya Mpira wa Pete ya Baraza La Wawakilishi kinaendelea kujiweka sawa kwa ajili  ya kujiandaa na Mashindano watakayoshiriki Msimu huu.

Akizungumza katika Kiwanja cha Mazoezi ya Timu hiyo Chukwani mara baada ya kukamilisha mazoezi Nahodha wa Timu hiyo Fatma Mandoba amesema Timu hiyo imejiandaa vizuri ili kuhakikisha wanafanya vyema kwa ajili ya kutimiza adhma waliyojiwekea ya kuibuka na Ubingwa katika Mashindano yote watakayoshiriki.

WANAFUNZI UMITASHUMTA KUHAKIKISHA WANARUDI NA USHINDI

Wanafunzi wanaoshiriki Mashindano ya umitashumta Kanda ya Unguja na Pemba wametakiwa kufanya jitihada za kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika Michuano hiyo inayofanyika Kitaifa Mkoani Tabora

Hayo yameelezwa na Afisa Mdhamini wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwenye Ziara ya kuwatembelea Washiriki hao kwa lengo la kujua matokeo ya michezo yao na changamoto zinazowakabili.

Nae Mkurugenzi wa Wizara ya ELimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Hafsa Abodtwalib amesisitiza Washiriki hao kuhakikisha wanatunza nidhamu zao. 

WASANII WA ZANZIBAR NA TANZANIA BARA KUSHIRIKIANA KATIKA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Ndg.Fatma Hamad Rajabu amesema mchanganyiko wa Wasanii wa Maigizo katika Tamthilia ya Mawio ni njia ya kudumisha Muungano wa Tanzania.

    Akizindua Tamthilia ya Mawio kwa niaba ya Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita huko N'gomekongwe amesema hatua hiyo ni pamoja na kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan katika kudumisha Muungano huo.

Subscribe to Michezo
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.