WAZIRI TABIA AMKABIDHI TUNZO YA HESHIMA MSANII WA TAARAB ASILIA FATMA ISSA

WAZIRI TABIA

     Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita amesema  kuwepo kwa Tunzo za Wasanii kuna saidia kuleta ari na ushindani katika Tathnia ya Muziki.

    Akizungumza katika Usiku wa Kilele cha Tunzo za Kimataifa za Zanzibar International Music Awards Mh.Tabia amesema hatua hiyo itawawezesha Wasanii kuwapa hadhi na Hamasa ya kufanya kazi ili waweze kuwania Tunzo hizo

    Mwenyekiti wa Kamati za Tunzo za Zanzibar Intrnational Music Award Ndg.Ramadhan Bukini amesema Tunzo hizo zimekua na tija ili kuomdoa malalamiko.

    Msanii aliyepata Tunzo nyingi katika Usiku huo amesema haikuwa rahisi hivyo ameiyomba Wizara na Waandaji wa Tunzo hizo kuzifanya kuwa endelevu.

     Tunzo mbali mbali zilitolewa kwa Wasanii waliowania na kushinda kupitia kazi zao ikiwemo Tunzo ya Mwanamuziki bora wa Chipukizi wa Mwaka ,Muimbaji bora Taarab  Kike Tabia Hassan, Tunzo  Wimbo bora Taarab Asilia ya Mwaka Muimbiji bora Kiume Mwaka, Mtayarishaji bora Muziki Mwanamuziki bora  Kike Zenji Fleva ambapo pia Waziri Tabia alipata nafasi ya kukabidhi Tunzo ya heshima kwa Mwanamuziki wa Taarab asilia Fatma Issa

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.