Michezo

YANGA YATWAA UBINGWA NGAO YA JAMII 2024

    Yanga Bingwa wa Kombe la Ufunguzi wa Ligi Kuu bara 'Ngao ya Jamii' msimu wa 2024/2025.

 

MANCHESTER CITY YATWAA UBINGWA WA NGAO YA JAMII

    Klabu ya Manchester City imetwaa ubingwa wa kombe la Ngao ya Jamii kwa kuifunga Manchester United 7-6 kwenye mikwaju ya penati baada ya mchezo huo kumalizika kwa  kwa sare ya 1-1.

 

MTAALA WA MICHEZO KUIBUA VIPAJI TUMBATU

Kurejeshwa Mtaala wa Masomo ya Michezo kwa Wanafunzi kutasaidia kuibua na kuimarisha vipaji vya Michezo mbali mbali katika jamii.

Wakizungumza katika Ziara ya Waandishi wa Habari katika Kisiwa cha Tumbatu,

Mratibu wa Michezo na utamaduni Wilaya Kaskazini 'A' Khamis Hija Mohammed na

Sheha wa Shehia ya Uvivini, Ngwali Sheha Haji, wamesema hapo awali kulikuwa na Wanafunzi waliojishughulisha na Michezo na kufanikiwa kushiriki vyema  mashindano mbali mbali.

MASHABIKI YANGA WAJITOKEZA KWA WINGI KWA MKAPA

     Mashabiki wa Timu ya Wananchi Yanga wajitokeza kwa wingi katika Dimba la Benjamin Mkapa kwa ajili ya kushuhudia Timu yao ikiminyana na Red Arrows ya Zambia katika kilele cha Wiki ya Mwananchi huku Wakitamba juu ya ubora wa Kikosi chao

TIMU ZA LUMUMBA KABADDI KUIBUKA KIDEDEA DHIDI YA TIMU ZA LUMUMBA

Wachezaji wa Mchezo wa Kabaddi wametoa wito kwa Jamii kuunga Mkono Mchezo huo ambao umekuwa na fursa mbalimbali sawa na michezo mengine ikiwemo kushiriki Mashindano nje ya Nchi.

Wakuzungumza baada ya Mechi ya kirafiki kati ya timu ya Kike na Kiume  ya Lumumba na Kidimni Wachezaji hao wamesema jambo linalowavunja Moyo ni kuona mchezo huo haupewi thamani kama Michezo mengine.

Kocha wa Mchezo huo Tamal Hassan Mahakki amesema ameamuwa kujitoa kufundisha mchezo huo nje ya Wilaya ya Mjini ili Vijana wa maeneo mengine nao waweze kunufaika.

KIWANI STAR YAIBUKA KIDEDEA DHIDI YA KISIMANI

Timu ya Kisimani imekubali Kipgo cha mabao Mawili  kwa Moja dhidi ya Timu ya Kiwani Star katika Mchezo wa Mpira wa Miguu uliofanyika katika Kiwanja cha Mauani  Wilaya ya Mkoani.

MASHABIKI NA WAPENZI WAELEZA MATARAJIO YAO MCHEZO WA NGAO YA HISANI

Kuelekea Mchezo wa ngao ya hisani wa  PBZ Yamle Yamle Cup 2024 ambao utakwenda kuwakutanisha uso kwa uso   Mabingwa wa Michuano hiyo Mboriborini na Timu ya Mazombi, Mashabiki na Wapenzi wa Soka Visiwani Zanzibar  wamelezea matumaini yao kulekea Mchezo huo huku wakipongeza Maandalizi mazuri ya Msimu huu wa Sita wa Mwaga Maji.

HISPANIA YANYAKUA UBINGWA WA EURO 2024

    Hispania imenyakua ubingwa katika michuano ya EURO 2024 baada ya kuichapa England mabao 2 - 1.

   Mabao ya Hispania yamefungwa na Nico Williams 47' na Mikel Oyarzabal 86' huku goli pekee la England likifungwa na Cole Palmer 73'.

    Fainali hiyo imepigwa katika dimba la Olympiastadion huko Berlin, Ujerumani.

    Hii ni mara ya nne kwa Hispania kunyakua ubingwa katika michuano hiyo na EURO na England yenyewe haijawahi kuchukua ubingwa hata mara moja katika michuano hiyo.

MSIMU WA SITA WA YAMLE YAMLE CUP KUTOA ZAWADI KWA SHABIKI BORA

   Ikiwa bado zimebaki Siku chache  kuchezwa Mechi ya Ngao ya Hisani itakayo Mkutanisha Mabingwa wa Michuano hiyo Timu ya Mboriborini ambayo itakwenda kumenyana na Timu ya Mazombi Mchezo ambao utapigwa katika Dimba la Mau.

   Ikimbukwe kuwa Msimu wa Sita wa  PBZ Yamle Yamle Cup  ni Msimu wenye mafanikio mengi ikiwemo kushirikisha Timu  32 ikiwemo Timu Nane kutokea Visiwani Pemba .

UBINADAMU KAZI IMEIADHIBU MBORIBORINI KWA PENALT

Timu ya Ubinadamu Kazi imeibuka na Ushindi wa 4 – 2  baaada ya kuiadhibu Timu ya Mboriborini kwa Mikwaju wa Penalti katika Mchezo maalumu   kuadhimisho ya Siku ya kupambana na Rushwa.

Mchezo huo uliokuwa na Ushindani mkali kwa kila Timu kutaka kuibuka na Ushindi na hadi dakika 90 za Mchezo timu  hizo zilitoka Sare ya bila kufungana na Mikwaju Penalti ikachukua nafasi yake. 

Baada kumalizika kwa Mtanange huo baadhi ya Wachezaji wamesema kuwa ni muhimu wa Michezo na mapambano ya Rushwa. 

Subscribe to Michezo
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.