Timu ya Kisimani imekubali Kipgo cha mabao Mawili kwa Moja dhidi ya Timu ya Kiwani Star katika Mchezo wa Mpira wa Miguu uliofanyika katika Kiwanja cha Mauani Wilaya ya Mkoani.
Wakizungumza baada ya Mchezo huo baadhi ya Wachezaji i wa Timu ya Kismani Haji Dadi Haji amedai kipigo hicho kimekuja kutokana na maamuzi yasio sahihi huku kocha wa Timu ya Kiwani Mussa Haji abdalla akisema walitamba kutokana na mazoezi mazuri pamoja na Wachezaji kusikiliza maelekezo ya viongozi wao
Akifungua Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kiwani Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja amempongeza Mbunge huyo kwa kuanda a Mashindano hayo ambayo yanalenga katika kuibua Vibaji vya Vijana .
Nae Mbunge wa Jimbo la Kiwani Abdalla Rashid Abadalla amesema lengo la kuandaa Mashindano hayo ni kuwapa hamasa Vijana kushiriki katika Michezo.
Jumla ya Timu kumi na Saba zimeshiriki katika Mashindano hayo katika Jimbo la Kiwani zikijumuisha wadi ya Kiwani na Mwambe.