DKT. MWINYI AFUNGUA VIWANJA VYA MATUMBAKU SPORTS COMPLEX
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kujenga miundombinu ya viwanja vya michezo ili kuwawezesha vijana kujiajiri kupitia michezo.
Akifungua viwanja vipya vya Matumbaku Sports Complex vinavyo jumuisha michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa wavu ,kikapu, mpira wa Pete na mpira miguu, Dkt. Mwinyi amesema Kutokana na ukuaji wa soko la Ajira Duniani kupitia michezo, Serikali imeona ipo haja ya kuimarishwa viwanja hivyo ili kukuza utalii na kuimarisha uchumi wa nchi.