Mwingereza Emma Raducanu anasema anahisi kuzaliwa upya wakati huu, akijiandaa kurejea tena kwenye tenisi huko Auckland baada ya miezi minane nje ya uwanja.
Bingwa wa US Open 2021 alicheza mechi tisa pekee mnamo 2023, akiwa nje ya uwanja tangu Aprili.
Raducanu, mwenye umri wa miaka 21, alifanyiwa upasuaji wa mikono yote miwili na kifundo cha mguu wake wa kushoto mwezi Mei, na ameshuka hadi nafasi ya 298 katika viwango vya ubora duniani.
Iwapo atashinda mechi yake ya kwanza huko Auckland, Raducanu -ambaye ameingia kwenye mchuano hiyo akiwa na kiwango cha ulinzi atamenyana na mchezaji wa zamani wa kwanza wa Denmark Caroline Wozniacki au Kiukreni Elina Svitolina katika raundi ya pili.
Lakini mchezaji huyo wa zamani nambari 10 duniani lazima apitie mchujo ili kufikia droo kuu ya Australian Open, huku mchuano wa kwanza wa Grand Slam wa 2024 ukianza Januari 14.