Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kujenga miundombinu ya viwanja vya michezo ili kuwawezesha vijana kujiajiri kupitia michezo.
Akifungua viwanja vipya vya Matumbaku Sports Complex vinavyo jumuisha michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa wavu ,kikapu, mpira wa Pete na mpira miguu, Dkt. Mwinyi amesema Kutokana na ukuaji wa soko la Ajira Duniani kupitia michezo, Serikali imeona ipo haja ya kuimarishwa viwanja hivyo ili kukuza utalii na kuimarisha uchumi wa nchi.
Amesema malengo ya Serikali ni kuona Zanzibar inatajika kimataifa kupitia michezo, hivyo amewataka wanamichezo kutumia viwanja hivyo ili kuendeleza vipaji vyao na kufika mbali.
Aidha Amesema dhamira ya Serikali ya kujenga viwanja vya michezo vyenye kujuisha viwanja vya michezo mbali mbali ni kutimiza azma yake ya kuwatengenezea fursa wanamichezo kujitangaza kimataifa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na mipango Sada Mkuya Salum, amesema uwekezaji mkubwa umefanywa na mfuko wa hifadhi ya jamii ZSSF hivyoWanastahili kupongezwa Kutokana na kuunga mkono juhudi za maendeleo yanayofanywa na Rais wa Zanzibar katika sekta mbali mbali ikiwemo ya michezo.
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema kuna haja kuundwa kwa uongozi thabit wa kuhakikisha wanatunza viwanja hivyo ili kuendelea kuwa Bora Na hatua za kisheria zitachukuwa kwa yoyote atakaebainika anaharibu miundombinu ya viwanja hivyo.
Mkurugenzi muendeshaji ZSSF, Nassor Shaaban Ameir,amesema ujenzi wa viwanja hivyo umejumuisha viwanja mbali mbali ikiwemo mpira miguu, wavu na kikapu ambavyo vina ubora wa hali ya juu.
Ufunguzi wa viwanja hivyo uliambana na mchezo wa mpira wa miguu ambapo timu ya Karume Boys chini ya umri wa miaka 15 iliwaadhibu timu ya ZSSF kwa mkwaju wa penalty wa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa Ufunguzi wa Viwanja hivyo.