ASEMA UWEPO WA AMANI KATIKA TAIFA NI KICHOCHEO CHA KUKARIBISHA WAWEKEZAJI KUANZISHA MIRADI YENYE TIJA.

Ameyasema hayo kwenye hafla ya uzinduzi wa Hoteli ya Ycona Luxury Resort huko Uroa Pongwe, amesema mafanikio ya kiuchumi yaliyofikiwa hadi sasa yametokana na amani na utulivu iliopo nchini.

Hivyo  amesema kutokana na kuwepo fursa zaidi za kiuchumi  ni vyema kuiunga mkono Serikali katika kufikia dhamira hiyo na ameipongeza ZIPA kwa mkakati wa kubuni miradi ya aina hiyo. 

REAL MADRID HAWAJAPOTEZA MECHI, KATI YA 18 WALIZOCHEZA

Vigogo wa La Liga, Real Madrid walipata ushindi mnono dhidi ya Mallorca kutokana na bao la kichwa la Antonio Rudiger.

 

Mallorca iligonga mbao mara mbili huku mpira wa kichwa wa Antonio Sanchez ukipita chini ya mwamba wa goli hadi langoni, huku Samu Costa pia akigonga nguzo kwa wageni.

Makosa hayo yalikuwa ya gharama kwani Rudiger alifunga kwa kichwa akiunganisha kona nzuri ya winga ya kushoto ya Luka Modric dakika ya 78.

Real sasa hawajafungwa katika michezo 18 katika mashindano yote wanayocheza.

KYLIAN MBAPPE ASEMA BADO HAJAAMUA KUONDOKA PARIS ST-GERMAIN.

Mshambulizi wa Paris St-Germain Kylian Mbappe anasema hajafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake wa kuondoka au kubaki PSG.

 

Mkataba wa nahodha huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 na mabingwa hao wa Ligue 1 unamalizika msimu wa joto na amekuwa akihusishwa pakubwa na kuhamia Real Madrid.

Mbappe aliiambia PSG mwezi Juni kwamba hatachukua chaguo kwa miezi 12 zaidi katika mkataba wake.

Akizungumza baada ya kuifungia PSG wakiichapa Toulouse mabao 2-0 na kutwaa taji la Mabingwa wa Ufaransa.

NAPOLI KUMKOSA ALEX MERET, MWEZI MMOJA KUTOKANA NA JERAHA

Mabingwa watetezi wa Serie A Napoli watamkosa mlinda mlango wa kimataifa wa Italia Alex Meret kwa angalau mwezi mmoja baada ya kuumia misuli ya paja.

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alipata jeraha hilo katika sare ya bila kufungana dhidi ya Monza Ijumaa iliyopita, huku uchunguzi ukionyesha kupasuka kwenye msuli wa paja la kushoto.

Ingawa klabu haikusema atakaa nje kwa muda gani, lakini kwa mujibu wa wataalamu, jeraha kama hilo kawaida huhitaji angalau wiki tano za kupona.

NYOTA WA NIGERIA WILFRED NDIDI KUIKOSA AFCON KUTOKANA NA JERAHA.

Matumaini ya Nigeria kupata taji la nne la Kombe la Mataifa ya Afrika yalipata pigo siku ya Jumatano huku kiungo mashuhuri Wilfred Ndidi akitolewa nje ya michuano hiyo.

 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alikosa ushindi wa 4-1 wa timu yake dhidi ya Huddersfield Town siku ya Jumatatu kutokana na jeraha ambalo halijatajwa.

Msemaji wa timu hiyo Babafemi Raji alisema nafasi ya Ndidi imechukuliwa na kiungo Alhassan Yusuf ambaye amekuwa kwenye kiwango kizuri na mabingwa wa Ubelgiji, Royal Antwerp.

BONDIA MWAKINYO KUSHUKA ULINGONI JANUARI 27, VISIWANI ZANZIBAR

Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo anatarajiwa kushuka ulingoni tena Januari 27, 2024 kwenye ukumbi mpya wa ndani ya New Amaan Complex visiwani Zanzibar kupambana na Bondia wa Zimbabwe, Enock Msambuzi kwenye pambano litakalofahamika kama pambano la #MtataMtatuzi 
 

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Bondia huyo amesema amejiandaa vyema kuja kuonesha burudani na mpambano mkali ambao utakuwa ni zawadi kwa mengi mazuri yaliyofanywa na Rais wa Zanzibar kwenye kuboresha miundo mbinu ya michezo Zanzibar.

SIMBA SC KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII ZANZIBAR

Klabu ya Simba SC, imetangaza rasmi kuisadia Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar kutangaza Utalii wa visiwa hivi, kwa kutembelea maeneo yenye vivutio vya Utalii pamoja na kuvaa Jezi zilizoandikwa 'Visit Zanzibar' katika michezo yao ya Michuano ya Kombe la Mapinduzi. 

Simba itaanza kuvaa Jezi zilizoandikwa 'Visit Zanzibar' kwenye Mchezo wao wa Pili dhidi ya Singida Fountain Gate unaotarajiwa kuchezwa kesho majira ya saa mbili na Robo usiku katika Uwanja wa New Amaan Complex. 

LUCAL BERALDO AJIUNGA NA PSG KWA MKATABA WA MIAKA MITANO

Beki wa kati wa Brazil Lucas Beraldo, anayejulikana kama 'The Joker' kwa tabia yake ya kucheka muda mfupi kabla ya mechi, alisajiliwa na mabingwa wa Ufaransa Paris Saint Germain. 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alitia saini kandarasi ya miaka mitano na PSG, na hivyo kuhitimisha kukaa kwa miaka mitatu huko Sao Paulo ambaye alishinda naye Copa do Brasil 2023.

Beraldo, ambaye anasema kucheka kabla ya mechi ni sehemu ya maandalizi yake ya kiakili, alisema kujiunga na PSG ni hatua kubwa kwa maisha yake ya soka.

DKT. MWINYI AAHIDI KUENDELEA KUIMARISHA MIUNDO MBINU YA MICHEZO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.. Hussein Ali, Mwinyi amesema viongozi wanadhamira njema ya kuleta maendeleo endelevu yatakayo inua hali za uchumi kwa wananchi na huduma za jamii.

 

 Dkt. Mwinyi amesema Serikali itaendelea Kuimarisha miundo mbinu kwa viwanja vya michezo  kwa kuinua vipaji vya mazoezi  ikiwemo  kufanya mazoezi ili kuimarisha afya ya akili na kukuza uchumi kwa jamii ajira utalii 

WAWILI WAKAMATWA KUHUSIKA NA KIFO CHA MWANARIADHA BENJAMIN KIPLAGAT

Polisi nchini Kenya wamewakamata watu wawili kuhusiana na mauaji ya  mwanariadha wa Uganda Benjamin Kiplagat kwa kutumia kisu.

 

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi wa eneo hilo Stephen Okal, alisema  Wanaume hao wawili wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 walikamatwa katika mji wa Rift Valley wa Eldoret.

Kiplagat mzaliwa wa Kenya alikuwa anaiwakilisha Uganda kimataifa katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi, ikiwa ni pamoja katika Michezo kadhaa ya Olimpiki na Mashindano ya Dunia.

Subscribe to Sports
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.