Kiungo wa zamani wa Manchester United na Chelsea, Nemanja Matiç raia wa Serbia amesema kuwa moja ya kitu kipya alichokutana nacho alipojiunga na klabu ya Man United ni suala la wachezaji wake kuchelewa mazoezini.
Matic ameeleza kuwa wakati akiwa Chelsea wachezaji wote walikuwa professional na walikuwa wakifika mazoezini kwa wakati lakini United ilikuwa tofauti licha ya kuwekwa adhabu ya faini kwa wale wanaochelewa.
Amesema kuwa katika kipindi chote akiwa na United wachezaji vinara zaidi kwa kuchelewa mazoezini walikuwa ni kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba na Winga wa Uingereza, Jadon Sancho.
featured
hot
trending
standard