BINGWA MTETEZI MICHUANO YA MAPINDUZI CUP AANZA NA SARE

Mchezaji wa Timu ya Mlandege akijaribu kuwahadaa walinzi wa Azam FC

Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Mapinduzi Cup, timu ya Mlandege imeshindwa kutamba mbele ya Azam FC ambao ndio mabingwa wa kihitoria wa michuano baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana katika mchezo wa ufunguzi wa Mashindano hayo kwa msimu huu, katika Uwanja wa New Amaan Complex.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza kilikua na vuta nikuvute kwa timu zote mbili, huku lango la Azam FC likionekana kushambuliwa sana katika dakika 45 za kipindi za kipindi cha pili, na kupelekea dakika 90' zikamilike kwa sare tasa ya bila ya kufungana.

Mchezo uliyofata wa michuano hiyo ya kombe la Mapinduzi saa 2:15 usiku, Chipukizi ya Pemba ilipowakaribisha Vitalo'o ya nchini Burundi katika Dimba la New Amaan Complex na mchezo huo kutamatika kwa sare tasa ya bila ya kufungana na kupelekea kugawana alama moja moja kwa kila timu.

Hatua hiyo inapelekea kuandikwa kwa historia ambapo mpaka hivi sasa toka Uwanja ufanyiwe Matengenezo makubwa, vyavu zake hazijaruusu bao la aina yoyote ile toka kuanza kwa mashindano kadhalika toka Ufunguliwe Uwanja huo jana jioni.

Michuano ya Mapinduzi Cup inatarajiwa kuendelea tena kesho, Disemba 29, 2023 KVZ wakiwakaribisha Jamhuri kutoka Pemba, saa 10:15 jioni na JKU wakiwakaribisha Singida FG ni saa 2:15 usiku.

hot
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.