Nyota wa klabu ya KVZ, Akram Mhina Omar ndie mchezaji wa kwanza kufunga bao katika Uwanja wa New Amaan Complex, baada ya matengenezo makubwa yaliyochukua takribani miezi Sita, katika mchezo wa michuano ya Mapinduzi Cup dhidi ya Jamhuri.
New Amaan Compex, ulifunguliwa rasmi Disemba 27, 2023 saa kumi na moja dakika 23 jioni, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi baada ya ukarabati huo kupita.
Ilichukua takribani mechi tatu kwenye dakika 270 kutokuingizwa bao lolote kwenye wavu la goli la Kusini na Kaskazini la Uwanja huo, ndipo jana Disemba 29, 2023 saa 10:27, Mshambuliaji wa KVZ, Akram Mhina akaitanguliza timu hiyo kwa bao maridadi na ndio historia inaandikwa kuwa ndio bao lwa kwanza kufungwa na mchezaji huyo baada ya matengenezo ya Uwanja.
Mechi zilizopita katika uwanja huo ambazo hazikuzalisha bao hata moja ni ile ya Zanzibar Heroes dhidi ya Kilimanjaro Stars, Mlandege dhidi ya Azam FC, na Chipukizi dhidi ya Vitalo’o ya Burundi.