TIMU YA MPIRA WA PETE YA BLW KINAJIANDAA NA MASHINDANO MSIMU HUU.

MICHEZO BARAZA LA WAWAKILISHI

Kikosi cha Timu ya Mpira wa Pete ya Baraza La Wawakilishi kinaendelea kujiweka sawa kwa ajili  ya kujiandaa na Mashindano watakayoshiriki Msimu huu.

Akizungumza katika Kiwanja cha Mazoezi ya Timu hiyo Chukwani mara baada ya kukamilisha mazoezi Nahodha wa Timu hiyo Fatma Mandoba amesema Timu hiyo imejiandaa vizuri ili kuhakikisha wanafanya vyema kwa ajili ya kutimiza adhma waliyojiwekea ya kuibuka na Ubingwa katika Mashindano yote watakayoshiriki.

Wachezaji wa Timu hiyo wamewaomba Wachezaji wenzao pamoja na Mashabiki wao  kuendelea kuwaunga Mkono kwa kushiriki katika Mazoezi ikiwa ni Mpango wa kuimarisha Kikosi hicho kutokana na umuhimu na ukubwa wa Mashindano wanayoshiriki ndani ya Mwaka huu.

Kwa Mwaka huu Timu ya mpira wa Pete ya Baraza la Wawakilishi imeshiriki  Bonanza Jumamosi ya Tarehe 8 Mwezi huu dhidi ya klabu ya Wazee Sport  ya Arusha katika Viwanja vya Mao na kupata Ushindi mzuri.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.