Akizingumza na Viongozi na Wachezaji wa Timu hizo katika Hafla ya Chakula cha Usiku kilichoandaliwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika Viwanja vya Hotel ya Verde Mtoni Zanzibar.
Kampuni ya kubashiri Michezo Sportpesa imeikabidhi Klabu ya Yanga Hundi yenye Thamani ya Milioni 537,500,00 ikiwa ni Bonus ya mafanikio ya Msimu 2023/2024 ambayo itawekwa kwenye Akaunti za Benki za Klabu hiyo.
Katika makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Sport pesa Tarimba Abbas amesema Sport Pesa inatimiza kile kilicho ahidi mwanzoni wa Msimu kwa Klabu hiyo kutiiza masharti ikiwemo kuchukua Ubingwa wa Ligi ya NBC Primer Ligue
Mamia ya Wananchi na Wanamichezo Visiwani Zanzibar wamejitokeza kuusindikiza Mwili aliyekuwa Kocha wa makipa wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes na Taifa Stars, Marehemu Saleh Ahmed maarufu Machupa.
Marehemu Saleh Machupa, amefariki Dunia Usiku wa kuamkia Leo Juni 3, 2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.
Feisal Salum ametoa Pongezi kwa Kiungo Mshambuliaji wa Yanga Azizi Ki kwa kuibuka Mfungaji bora katika Ligi Kuu ya NBC Premium League baada ya kupachika Magoli 21.
Ikumbukwe kuwa nafasi hiyo ya Ufungaji bora ilikuwa ikigombaniwa na Viungo Wawili hao huku Azizi Ki na Fei Toto ambapo Aziz Ki akitupia Jumla ya Mabao 21.
Chama Cha netball Zanzibar kimefungua Dirisha la uchukuaji Fomu za kuwania nafasi mbali mbali ikiwemo nafasi ya Uraisi wa Chaneza Taifa.
Akizungumza na Waandishi wa habari katika Ofisi za Baraza la Taifa la Michezo, Mwanakwerekwe, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Muhidini Masuzu, amesema uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Tarehe 9 Mwezi 6.
Timu ya Tanzania ya wavulana imefuzu hatua ya fainali ya mashindano ya Mabingwa kwa Shule za Afrika (ASFC) kwa mwaka 2024 yanayofanyika visiwani Zanzibar.
Wamefuzu baada ya kupata ushindi dhidi ya Benin kwa magoli 2-0 katika mchezo uliochezwa Mei 23,2024.
Fainali itachezwa dhidi ya Guinea ambayo imepata ushindi kwa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya Senegal baada ya kutoa suluhu kwa dakika 90.
Fainali hio itachezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex-Zanzibar, Mei 24,2024.
Timu ya JKU ya Mpira wa Mikono imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Kombe la mwenge CUP baada ya kuicharaza mabao 25 kwa 16 Timu ya Nyuki Mchezo wa fainali ulivurumishwa katika Uwanja wa Jeshini.
Mchezo huo ulikuwa na vuta nikuvute kwa kila timu kutaka kuwa Bingwa lakini Nyuki walishindwa kufua Dafu mbele ya jku na kuruhu Timu hiyo kuondoka na Vikombe kwa upande wa Wanawake na Wanaume.
Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba, Mfamau Ali Mfamau amesema Viongozi wa Nchi wamekua wakiwekeza katika Viwanja vya Michezo kwa kujenga Viwanja vya Kisasa zaidi.
Mdhamini Mfamau ameyaleza hayo katika Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Michezo na Maendeleo, unaotekelezwa na Kituo cha Majadiliano kwa Vijana Zanzibar (CYD kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Wizara ya Elimu na Wizara ya Maendeleo ya Jamii jinsi kwa ufadhili wa Shirika la Ujerumani (GIZ).
Waziri Tabia ametoa kauli hiyo, alipofungua Rasmi Mashindano ya Kimataifa ya CAF Afrika Schools kwa Wasichana na Wavulana yanayofanyika Uwanja wa New Amaan Complex.
Amesema juhudi za Mashirikisho ya Mpira zimesaidia Zanzibar kuendelea kutajika Kimataifa kwani Mashindano hayo yamekuwa Chachu ya Utalii wa Kimichezo Nchini.
Klabu ya Manchester City imetwaa Ubingwa wa English Premier League (EPL) baada ya kuifunga klabu ya West Ham United magoli 3-1 na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kubeba kombe hilo kwa mara nne mfululizo bila kupokeza kijiti hiko kwa klabu nyingine.
Manchester City inachukua ubingwa baada ya kufikisha pointi 91, ikifuatiwa na klabu ya Arsenal yenye alama 89 baada ya kushinda magoli 2-1 dhidi ya Everton katika michezo ya kukamilisha msimu wa 2023/24 Mei 19,2024