Timu ya JKU ya Mpira wa Mikono imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Kombe la mwenge CUP baada ya kuicharaza mabao 25 kwa 16 Timu ya Nyuki Mchezo wa fainali ulivurumishwa katika Uwanja wa Jeshini.
Mchezo huo ulikuwa na vuta nikuvute kwa kila timu kutaka kuwa Bingwa lakini Nyuki walishindwa kufua Dafu mbele ya jku na kuruhu Timu hiyo kuondoka na Vikombe kwa upande wa Wanawake na Wanaume.
Makepteini wa Timu zote mbili wamesema Mchezo umeenda Vizuri hivyo wamewataka waandaaji wa Mashindano hayo kuweka Mikakati ya kuhakikisha ligi hizo zinakua endelevu .
Keptein JKU Iddi Haji na Muandaaji wa Mashindano hayo Khalfan Seif wametaka Wananmichezo kuungamkono juhudi za Serikali katika kukuza na kuinua Michezo Nchini.
Katika Mashindano hayo Mshindi wa kwanza JKU alikabidhiaa Vikombe na Vifaa vya kuchezea huku Timu zote Shiriki zikabidhiwa Zawadi ya Mpiara.