Michezo

WASIMAMIZI UCHAGUZI WATAKIWA KUFUATA MIONGOZO YA TUME

    Wasimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kwahani wamesisitizwa kutenga muda wao kusoma Katiba Sheria na Muongozo wa Tume ili kuhakikisha Wanafanya kazi kwa uhakika na kuendesha Uchaguzi wa haki

     Akifunga Mafunzo ya Wasimamizi hao Makamo Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC  Jaji Mbarouk Salim Mbarouk amesema jukumu walilopewa linahitaji umakinii hivyo kujituma kwao kutasaidia kuendesha Uchaguzi Wente mafanikio

TP MAZEMBE YAVUTIWA NA MAFANIKIO YA YANGA.

Mabingwa wa Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara   Young Africa  wamesema ujio wa Ujumbe wa  Klabu ya TP Mazembe kuja kujifunza kwao kutaleta heshima  katika Klabu hiyo.

Viongozi wa Klabu ya Yanga wamesema  ni heshima kubwa kwa Klabu hiyo kutoka Congo kuja kujifunza kwao mambo mbali mbali ikiwemo masuala ya Uongozi na namna ya kuendesha Klabu hiyo kupitia Wanachama.

Kiongozi wa Ujumbe huo kutoka Klabuya TP Mazembe amesema wamevutiwa na mafanikio makubwa ya Klabu hiyo hivyo ujio wao utasaidia kuleta  tija katika Klabu yao.

DKT.MPANGO AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 79 BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

     Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania inatambua michezo ya majeshi ni nguvu kubwa ya kidiplomasia inayovuka mipaka na kuimarisha uhusiano baina ya mataifa Duniani.

YANGA SC YATWAA UBINGWA WA 30 LIGI KUU TANZANIA BARA 'NBCPL'

      Yanga Sc yatwaa ubingwa wa NBC Premier League kwa mwaka 2023/24 wakiwa wamebakisha mechi tatu ili kukamilisha ratiba ya Ligi kuu

       Hii ni kutokana na matokeo waliyopata leo dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo inafanya wafikie pointi 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kati ya zilizo chini yao katika msimamo wa ligi kuu

      FT: Mtibwa Sugar 1⃣-3⃣ Yanga Sc

      Huu ni ubingwa wao wa tatu mfululizo na ni wa 30 kwao kwenye ligi kuu Tanzania Bara.

 

REAL MADRID YATWAA UBINGWA WA LALIGA 2023/2024

    Real Madrid imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uhispania (LaLiga) ikiwa imesaliwa na michezo minne mkononi baada ya kushinda magoli 3-0 dhidi ya Cadiz.

   Baada ya Madrid kutangazwa mabingwa wa La Liga nafasi ya pili inashikwa na Girona FC yenye alama 74 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Barcelona yenye alama 73, timu zote zikiwa zimecheza michezo 34.

 

SERIKALI KUJENGA VITUO VYA MICHEZO UNGUJA NA PEMBA

     Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita amesema Serikali ina mpango wa kuimarisha miundo mbinu ya Michezo kwa kujenga Vituo vya Michezo Academy kwa kila Mkoa Unguja na Pemba.

    Waziri Tabia ametoa kauli hiyo, wakati akiwaaga Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Wasichana ya Zanzibar Spark, inayotarajia kushindana katika Mshindano ya Mpira wa Miguu ya Kimataifa Nchini Ufaransa.

DKT.NDUMBARO AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMUSTA

     WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Chama cha Maafisa Utamaduni na Sanaa Tanzania (CHAMUSTA) na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo suala la kukabiliana na mmomonyoko wa maadili katika jamii, uboreshaji wa mazingira ya utendaji kazi ya maafisa utamaduni pamoja na ubidhaishaji wa urithi wa utamaduni kwa ajili ya utalii wa utamaduni, Malikale na michezo.

WADHAMINI WAMEOMBWA KUENDELEA KUWASAIDIA WANAMICHEZO

Viongozi na Wanamichezo mbali mbali wameshauriwa kuendelea kuweka jitihada kwenye kukuza Michezo kwa kuzisaidia Timu ili ziweze kujikwamua Kiuchumi.

Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Taasisi Afrocare Phamasi, Grace Edgar wakati wakikabidhi vifaa vya Michezo kwa Timu ya Jamhuri FC,   amesema kudhamini wao utahakikisha Vijana Wanacheza Mpira wakiwa na Afya njema ili kuweza kufanya vizuri katika Michezo yao

Kocha Mkuu wa Timu hiyo, Ramadhani Abrahman Madundo amesema kukosekana kwa  udhamini kulichangia Timu yake kutokufanya vizuri kwenye Mashindano.

KATIBU BARAZA LA MICHEZO AKUTANA NA UONGOZI WA TAASIS YA 'ZYBA'

       Katibu Mtendaji Baraza la Michezo Zanzibar, Said Kassim amekutana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Zanzibar Youth Basketball (ZYBA) Abdul Azizi Salim na kutoa Baraka za Mashindano ya ZYBA BASKETBALL 2024, yatakayoanza hivi karibuni.

     Viongozi wa Baraza wameipongeza ZYBA kwa kuweza kuandaa jambo kubwa na zuri lakini pia litakaloweza kuitangaza Zanzibar Kimichezo.

TANZANIA YAINGIA MAKUBALIANO NA IVORY COAST KATIKA SEKTA YA MICHEZO

     Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeingia makubaliano ya ushirikiano na Wizara ya Michezo ya Ivory coast  katika masuala mbalimbali ya uendelezaji wa Sekta ya michezo.a                   

Subscribe to Michezo
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.