SERIKALI KUJENGA VITUO VYA MICHEZO UNGUJA NA PEMBA

Waziri Tabia

     Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita amesema Serikali ina mpango wa kuimarisha miundo mbinu ya Michezo kwa kujenga Vituo vya Michezo Academy kwa kila Mkoa Unguja na Pemba.

    Waziri Tabia ametoa kauli hiyo, wakati akiwaaga Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Wasichana ya Zanzibar Spark, inayotarajia kushindana katika Mshindano ya Mpira wa Miguu ya Kimataifa Nchini Ufaransa.

    Waziri Tabia amesema ujenzi wa Vituo hivyo utasaidia kuongeza Wachezaji Wenye Vipaji, Nidhamu na tabia njema huku akiitaka Timu hiyo kuwa na ari na hamasa na kutafuta ushindi.

     Kamishna wa Idara ya Michezo Zanzibar, Ameir Mohamed Makame amesema Sera ya Michezo, ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na Dira ya Maendeleo imesisitiza ushiriki wa Michezo kwa jinsia zote.

    Timu ya Wasichana chini ya Umri wa Miaka 14 ya Zanzibar Spark, inatarajiwa kwenda kushinda Mashindano ya Vijana kuanzia Mei 7 hadi 16 Jijini Paris Nchini Ufaransa.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.