Mabingwa wa Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara Young Africa wamesema ujio wa Ujumbe wa Klabu ya TP Mazembe kuja kujifunza kwao kutaleta heshima katika Klabu hiyo.
Viongozi wa Klabu ya Yanga wamesema ni heshima kubwa kwa Klabu hiyo kutoka Congo kuja kujifunza kwao mambo mbali mbali ikiwemo masuala ya Uongozi na namna ya kuendesha Klabu hiyo kupitia Wanachama.
Kiongozi wa Ujumbe huo kutoka Klabuya TP Mazembe amesema wamevutiwa na mafanikio makubwa ya Klabu hiyo hivyo ujio wao utasaidia kuleta tija katika Klabu yao.
Klabu ya Yanga ni Mabingwa wa Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara mara Tatu mfululilizo na Taji la 30 la Ligi Kuu ikifuatiwa na Simba iliyotwaa 22 , Yanga pia tayari imejihakikishia kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika Msimu ujao.
stories
standard