WASIMAMIZI UCHAGUZI WATAKIWA KUFUATA MIONGOZO YA TUME

WASIMAMIZI UCHAGUZI MDOGO

    Wasimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kwahani wamesisitizwa kutenga muda wao kusoma Katiba Sheria na Muongozo wa Tume ili kuhakikisha Wanafanya kazi kwa uhakika na kuendesha Uchaguzi wa haki

     Akifunga Mafunzo ya Wasimamizi hao Makamo Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC  Jaji Mbarouk Salim Mbarouk amesema jukumu walilopewa linahitaji umakinii hivyo kujituma kwao kutasaidia kuendesha Uchaguzi Wente mafanikio

    Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Ramadhan Kailima amesema matarajio ya Tume hiyo ni Uchaguzi huo kwenda vizuri na kupata matokeo bora

    Msimamizi Uchaguzi Jimbo la Kwahani Safia Iddi Muhammad amesema Ushiriki wao katika Mafunzo hayo watahakikisha Wanayafanyia haki katika kufuata miongozo na maelekezo ya Tume 

    Uchaguzi wa Nafasi ya Ubunge Jimbo la Kwahani unatarajiwa kufanyika June 8 

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.