Viongozi na Wanamichezo mbali mbali wameshauriwa kuendelea kuweka jitihada kwenye kukuza Michezo kwa kuzisaidia Timu ili ziweze kujikwamua Kiuchumi.
Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Taasisi Afrocare Phamasi, Grace Edgar wakati wakikabidhi vifaa vya Michezo kwa Timu ya Jamhuri FC, amesema kudhamini wao utahakikisha Vijana Wanacheza Mpira wakiwa na Afya njema ili kuweza kufanya vizuri katika Michezo yao
Kocha Mkuu wa Timu hiyo, Ramadhani Abrahman Madundo amesema kukosekana kwa udhamini kulichangia Timu yake kutokufanya vizuri kwenye Mashindano.
Mdhamini wa maendeleo Kijiji cha Makunduchi, Muhammed Simba Hassan amesema tayari Udhamini utafungua fursa kwa vijana kuonesha vipaji vyao.
Timu ya Jamhuri ya Makunduchi inashiriki Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Unguja.