Mamia ya Wananchi na Wanamichezo Visiwani Zanzibar wamejitokeza kuusindikiza Mwili aliyekuwa Kocha wa makipa wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes na Taifa Stars, Marehemu Saleh Ahmed maarufu Machupa.
Marehemu Saleh Machupa, amefariki Dunia Usiku wa kuamkia Leo Juni 3, 2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.
Marehemu Machupa aliwahi kucheza Timu ya Miembeni na kufundisha baadhi ya Vilabu mbali mbali ikiwemo Black Saler, Timu ya Taifa ya Zanzibar Zanzibar Heroes na Timu ya Taifa ya Tanzania taifa Stars hadi Mauti yanamfika Marehe Machupa alikuwa akifundisha Timu ya Geita gold.
Baadhi ya Wachambuzi na Waandishi wa Michezo Zanzibar walielezea umahiri na mchango wake katika Tasnia ya Michezo Zanzibar na Tanzania.
Marehemu Machupa pia aliwahi kuwa Mkufunzi wa Kimataifa wa Makipa Nchini TAnzania akifundisha Kozi na Mafunzo mbali mbali kwenye Tasnia ya Michezo.
Marehemu Machupa amezikwa Leo Majira ya Saa Saba Mchana katika Kijiji ch Kinyasini, Mkoa wa Kaskazini.
Innallah Waina Ilah Rajiun,hakika Sisi ni wa MUNGU na kwakwe tutarejea.