TIMU YA TAIFA YA KABADDI KUELEKEA KENYA MICHUANO YA KIMATAIFA

WANAMICHEZO

   Balozi wa India Nchini Dk. Kumar Praveen amesema ataendelea kuunga mkono Mchezo wa Kabaddi ili uweze kukuwa na kuipeperusha Bendera ya Zanzibar Kimataifa kupitia Mchezo huo wenye asili ya Kihindi. 

    Akizungumza katika Shamra shamra za Siku ya Yoga Kimataifa inayotarajiwa kuadhimishwa June 21 Balozi Kumar amesema Mazoezi na Michezo ni Afya na Ajira hivyo kuunga mkono juhudi za Vijana hao ni kuwasaidia kuwajenga Kiakili, Kiafya na kuwasogeza kufikia ndoto zao.

   Amesema ana imani kubwa na Timu hiyo ya Taifa kwenda kuiwakilisha vyema Zanzibar na kurudi na ushindi kutokana na maandalizi mbalimbali aliyoyashuhudia na ari ya Vijana hao.

    Wajumbe wa Shirikisho la Mchezo wa Kabaddi Zanzibar  wamewashukuru Wadau waliojitokeza kuidhamini Timu hiyo kwenda kushiriki Mashindano ya Kabaddi Afrika Nchini Kenya. 

   Jumla ya Nchi Kumi za Afrika zimethibitisha kushiriki Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza June 21 Hadi 30.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.