WASANII WA ZANZIBAR NA TANZANIA BARA KUSHIRIKIANA KATIKA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA

KATIBU WIZARA YA HABARI

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Ndg.Fatma Hamad Rajabu amesema mchanganyiko wa Wasanii wa Maigizo katika Tamthilia ya Mawio ni njia ya kudumisha Muungano wa Tanzania.

    Akizindua Tamthilia ya Mawio kwa niaba ya Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita huko N'gomekongwe amesema hatua hiyo ni pamoja na kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan katika kudumisha Muungano huo.

   Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Sensa ya Filamu na Utamaduni Juma  Chum Juma amesema thamani ya Wasanii ni kubwa kupitia kazi zao hivyo aliwataka kuendelea kudumisha Vipaji vyao . 

   Msanii Salim Ahmed (Gabo Zigamba) ametoa shukrani kwa Wafadhili waliowasaidia pamoja na Wasanii wote kwa kujitoa kwao ili kuhakikisha wanafanikisha Tamthilia hiyo.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.