JAMII YAKUMBUSHWA KUTUNZA AFYA KWA KUFANYA MAZOEZI

MLEZI WA BARAFU JONGING

Jamii imekumbushwa kuendelea kufanya Mazowezi na kutunza Mazingira ili kuimarisha afya zao.

Akizungumza mara baada ya Matembezi ya Kilomita Sita na Bonaza la Mazowezi Mlezi wa Barafu Jonging Iddi Azan amesema kufanya Mazowezi ni muhimu kwa Afya na amewataka Vijana kuacha kutumia Vileo ambavyo vinaharibu Maisha yao.

Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara ya Afya Dkt. Ntuli Kapologwe amesema Wizara ya Afya inampango mkakati wa kuimarisha afya ya Jamii kwa kutumia Mabonaza ambayo yanashirikisha Jamii moja kwa moja.

Nao Washiriki wa Bonaza hilo Vikiwemo Vikundi vya Mazowezi cha Maisara na Obama vya Zanzibar wamesema kuwa ushirikiano kwa Michezo Tanzania Bara na Zanzibar ni kuimarisha Muungano na Afya zao.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.