KWEREKWE BINGWA MICHUANO YA FA WILAYA YA MAGHARIBI B

TIMU YA MWANAKWEREKWE BINGWA

Timu ya Mwanakwerekwe Bingwa Michuano ya FA Wilaya ya Maghari B baada ya kuyadhibu Timu ya Fuoni kwa Bao 1-0 katika Mchezo wa Fainali ya Michuano hiyo.

Michuano hiyo iliyochezwa katika Dimba la Mau ambapo Timu ya  Kwerekwe iliyo Valia Jezi rangi Nyeusi walionesha ufundi wao wa kutafuta goli katika dakika za mapema na hadi  kipenga cha Mwisho cha muamuzi kupigwa Fuoni  ilishindwa kuonesha uhodari wake na kuamuru Ubingwa huo kwenda kwa Kwerekwe.

Maulid Sheria Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Miguu Wilaya ya Magharib amesema Michezo niajira hivyo uwepo wa Ligi hiyo inasaidia kukuza nakuibua Vipaji

Bingwa Michuano hiyo alikabidhiwa kitita cha Fedha Taslim  pamoja na kukabidhiwa Vifaa vya michezo ambapo pia bingwa wa Daraja la Pili Timu ya Kinuni City alikabidhiwa Zawadi.

standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.