Habari

JUMUIYA YA SHIA YAMPONGEZA DKT.MWINYI KWA KAZI NZURI ANAZOFANYA

      Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameushukuru uongozi wa Jumuiya ya Shia Tanzania kumpongeza kwa kazi nzuri anazozifanya kuwaletea maendeleo makubwa wananchi wa Zanzibar.

     Rais Dk.Mwinyi ametoa shukrani hizo alipokutana na Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania, Maulana Sheikh Hemedi Jalala na ujumbe wake Ikulu Zanzibar .

      Aidha Rais Dk.Mwinyi ameiomba Jumuiya hiyo kuendelea kuiomba Dua nchi kuidumisha katika amani na utulivu.

WAZIRI PEMBE ASISITIZA JUU YA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WASICHANA ILI KUWAKINGA NA MIMBA ZA UMRI MDOGO PAMOJA NA MAAMBUKIZI YA MARADHI MBALIMBALI

    Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amesema kuna umuhimu mkubwa wa kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa wasichana ili kuwaepusha na mimba za umri mdogo pamoja na maambukizi ya maradhi mbalimbali.

     Akizungumza katika sherehe ya siku ya Hedhi Salama Duniani, iliyoadhimishwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya WAJAMAMA na Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, huko Mbweni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, amesema afya ya uzazi kwa wasichana ni muhimu kwani inawasaidia kujitambua na kuepukana na vishawishi.

WAZIRI MKUU KUFANYA ZIARA YA SIKU TATU MKOANI GEITA

     Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu (3) mkoani Geita kwa lengo la kushiriki Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira ambapo kikanda yatafanyika mkoa wa Geita, na kimkoa yamepangwa kufanyika wilayani Chato.

JKCI KUPATA IHIBATI YA MAABARA

Maabara ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)imepata ithibati ya viwango vya ubora wa Kimataifa katika kutoa huduma za Vipimo vya Magonjwa ya moyo na Magonjwa mengine.

Ithibati hiyo iliyotolewa na Shirika la kimatifa la viwango iso kufuatia JKCI kukidhi Vigezo vyote vilivyowekwa na Shirika hilo ikiwemo kuwa na Mashine za kisasa zinazotoa Vipimo zaidi 86 vya Uchunguzi wa Magonjwa mbali mbali yakiwemo ya moyo.

MAKUMBUSHO KUKUZA UTALII NA UCHUMI WA ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Makumbusho ya Amani na Viumbe hai yatasaidia kukuza Sekta ya Utalii na Uchumi wa Nchi kwa vile ni Kivutio kikubwa cha Wageni wanaoitembelea zanzibar.

RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA NCHINI KOREA .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya Ziara ya kikazi ya siku 6 Nchini Korea ikiwa ni mwaliko wa wenyeji wake Rais wa Taifa hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Mkamba amesema ziara hiyo inatarajiwa kuanza May 30 hadi Juni 6 mwaka huu ambapo pia Rais Dkt Samia anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Korea.

AMEND NA UBALOZI WA USWIS WAMEFANIKIWA KUWEKA MIUNDOMBINU YA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI

Katika jitihada za kupunguza Ajali za Barabarani kwa Wanafunzi Nchini Jijini Tanga, Shirika la Amend kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uswis wamefanikiwa kuweka Miundombinu alama za Usalama Barabarani yenye lengo la kuhakikisha Wanafunzi wanavuka salama katika Safari ya kwenda na kurudi Shuleni.

BAADHI YA HOSPITALI HAZINA SIFA YA HUDUMA YA MFUKO WA BIMA YA AFYA

Wizara ya Afya   imesema huduma  za Mfuko wa Bima ya Afya Zanzibar  hazipatikani katika baadhi ya Hospitali  kutokana na Hospitali hizo  kutokukidhi vigezo  vya kutoa huduma kwa Wnachama wake.
Naibu waziri wa  Wizara hiyo Mh Hassan Khamis Hafidhi amesema   sababbu  nyengine  zinatokana na  kuwepo kwa upunbgufu wa Madaktari, Dawa pamoja na kutokuwa na Vifaa Tiba katika baadhi ya Hospitali.

WANANAKE WATAKIWA KUZIDISHA USAFI KIPINDI CHA HEDHI ILI KUJIKINGA NA MARADHI

    Katika kuadhimisha Siku ya Hedhi Salama Duniani Wanawake wametakiwa kuzidisha usafi kwenye kipindi hicho ili kujinga na magonjwa mbalimbali yanayoweza kujitokeza.

    Ushauri ho umetolea na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kinamama Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Dk.Fatma Said Mohamed wakati akizungumza na ZBC katika Siku ya Hedhi Salama Duniani.

ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 200 ZAHITAJIKA KUREKEBISHA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MADARAJA

     Zaidi ya Shilingi Bilioni 200 zinahitajika kwa ajili ya marekebisho ya miundombinu ya Barabara na Madaraja yaliyo athiriwa na Mvua kubwa zilizonyesha Nchini kote.

     Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Miundombinu kutoka Ofisi ya Raisi Tamisemi Mhandisi Rogatus Hussein Mativila amebainisha hilo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam na kusema kuwa tayari tathmini ya uharibifu uliotokea imeshafanyika na wanachosubiria ni kutengemaa kwa Hali ya Hewa.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.