Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Miundombinu kutoka Ofisi ya Raisi Tamisemi Mhandisi Rogatus Hussein Mativila amebainisha hilo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam na kusema kuwa tayari tathmini ya uharibifu uliotokea imeshafanyika na wanachosubiria ni kutengemaa kwa Hali ya Hewa.
Mhandisi Mativila amesema Asilimia 2 Pekee ya Mtandao wa Barabara zilizo chini ya Tarura ziko katika kiwango cha Lami na zilizobakia ni Kiwango cha Udongo na Changarawe hivyo hawawezi kufanya marekebisho wakati ambao Mvua zinaendelea kunyesha kwani kufanya hivyo ni kutekeketeza Pesa za walipakodi.
Msimamizi wa Teknolojia mbadala wa Tarura Mhandisi Mshauri Fares Ngereja amesema Tarura imejipambanua kujenga Miundombinu ya Barabara na Madaraja kupitia Teknolojia mbadala ya matumizi ya Mawe badala ya Zege lengo likiwa ni kipunguza gharama za Ujenzi.
Wakala ya Barabara Mijini na Vijini Tarura ni moja ya Taasisi zinazoshiriki Kongamano la 30 la Shirikisho la Wahandisi Washauri linaloendelea Jijini Dar es salaam