Habari

MAISHA BORA FOUNDATION KUIMARISHA AFYA ZA WANAWAKE

    Taasisi ya Maisha Bora Foundation wametiliana Saini na Jumuiya ya Jamii na Watoto Wajamama kwa lengo la kutekeleza Majukumu ya pamoja ikiwemo  kuwaongezea hifadhi kina Mama na Wasichana wanapokuwa katika ada zao za Mwezi

    Afisa Mtendaji Mkuu wa Zanzibar Maisha Bora Foundation Ndg.Fatma Fungo amesema wameamua kushirikiana kwa pomoja ili kuhakikisha Wanawake na Watoto wanaimarisha Afya zao

SERIKALI KUENDELEA KUTHAMINI MCHANGO WA ASASI ZA KIRAIA

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Dkt. Saada Mkuya Salum, amesema Serikali inathamini mchango wa Asasi za Kiraia kama ni Wadau Wakuu wa shughuli za Maendeleo Nchini.

    Akifungua Mafunzo kwa Wadau wa Asasi za Kiraia kupitia mradi wa Uraia wetu huko Mazizini, amesema kupitia juhudi zao wamekuwa wakiunganisha Jamii kwa kuwafikia Wananchi kwa kiasi, kupitia shughuli muhimu ambazo Serikali iliwajibika kufanya hivyo.

ZMOTION NA TIGO PESA KUANZISHA MFUMO WA LIPA ADA NA SKULI BINAFSI

    Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh.Lela Mohammed Mussa amewaomba Wamiliki wa Skuli Binafsi kukaa pamoja na Wazazi kwa ajili   ya ulipaji Ada ya Masomo pindi Mwanafunzi anapochelewa kulipiwa Ada hiyo.

    Akizindua huduma ya Lipa Ada kwa Skuli Binafsi Waziri Lela amesema huo ni ubunifu wa Teknolojia  ambao utarahisisha  kutumika utendaji  katika Sekta ya Elimu.

WAZIRI NAPE ASISITIZA MATUMIZI YA AKILI MNEMBA (AI) KATIKA KUONGEZA UZALISHAJI NA UFANISI

      Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.), ametembelea banda la maonesho la kampuni ya ZTE linaloonyesha mafanikio makubwa ya matumizi mbalimbali ya Akili Mnemba (AI) na Mtandao wa Vitu (IoT), katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano Geneva, nchini Uswisi.

WATUHIMIWA 251 WAKAMATWA KWA VITENDO VYA UHALIFU MKOA WA MJINI MAGHARIB

     Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amesema jumla ya watuhumiwa 251 wamekamatwa kufuatia operesheni maalum ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu hapa Nchini.

       Ameyasema hayo huko katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Vuga wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali.

WIZARA YA MAJI KUWACHUKULIA HATUA WAKANDARASI WA MAJI.

Wizara ya Maji imeanza kuchukuwa hatua kwa Wakandarasi wanaoshindwa kukamilisha kwa wakati Ujenzi wa Miradi ya Maji kwa Wananchi.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Andrea Mathew, ametoa kauli hiyo wakati wa Ziara yake ya kukagua Miradi ya Maji, huko chemba Mkoani Dodoma.

Aidha, Waziri Kundo amesema Serikali imeendelea kutoa Fedha kwa ajili ya kusogeza huduma za Maji Karibu na Makazi ya Wananchi.

Baadhi ya Wananchi wa Jimbo la Chemba Mkoani Dodoma, wameishukuru Serikali kwa kuimarisha huduma za maji maeneo ya Pembezoni.

WAHANDISI WASHAURI KUSIMAMIA MIRADI NDANI YA BARA LA AFRIKA.

Makamo wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Philip Isdori Mpango amekitaka Chama cha Wahandisi Washauri TAnzania ACET  kuwandaa Wahandisi Washauri ili wawe na uwezo wa kusimamia Miradi mikubwa inayotekelezwa Nchi za Bara la Afrika.

WEMA KUSHAURIWA KUIPA UMUHIMU ELIMU MJUMUISHO

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameishauri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kulipa umuhimu  suala la elimu Mjumjuisho ili kuwajengea Mazingira mazuri ya Masomo Wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Wamesema pamoja na kujengewa Skuli  zenye mahitaji yao lakini bado hazionyeshi kukidha  mahitaji ya Watu wa aina hiyo.

WATANZANIA KUSHIRIKI KAMPENI YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulurhaman Kinana amewataka Watanzania kushiriki katika Kampeni ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia yenye lengo la kutokomeza matumizi ya Mkaa na Kuni ili kuhifadhi Mazingira 

MAMLAKA YA MJI MKONGWE YAWATAKA WANANCHI KUIMARISHA USAFI KATIKA MAENEO YA MJI HUO

    Mamlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar, imewataka Wananchi kuimarisha usafi wa mazingira  kwa lengo kuiweka haiba nzuri ya Mji sambamba na  kukuza Utalii Nchini.

   Mkurugenzi Idara ya Elimu Tafiti na Uwekezaji Mamlaka ya Mji Mkongwe, Ndg.Asha Ali Hassan ametoa wito huo wakati wa harakati wa usambazaji wa Vifaa vya kuhifadhia taka  huko Malindi amesema Mji Mkongwe ni kivutio kikubwa cha Watalii ambao kwa  asilimia kubwa unachangia kukuza pato la nchi kupitia sekta ya utalii.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.