Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameishauri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kulipa umuhimu suala la elimu Mjumjuisho ili kuwajengea Mazingira mazuri ya Masomo Wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Wamesema pamoja na kujengewa Skuli zenye mahitaji yao lakini bado hazionyeshi kukidha mahitaji ya Watu wa aina hiyo.
Wakiichangia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali katika Kikao kilicho endelea leo cha baraza la wawakilishi wajumbe hao wamesema uwepo wa Elimu mjumuisho bado halija fanikiwa ipasavyo ukilinganisha na Mhitaji ya Wanafunzi.
Wamesema suala hilo linahitaji kupewa kipaumbele na Wizara kuandaa Mitaala maalum itakayowasaida Wanafunzi kuondokana na vikwazo katika kupata Elimu ya lazima.
Aidha wameshuri kwa kusema ipo haja kwa wizara ya Elimu kulipa umuhimu wa kuandaa sera maalum zitakazo simamia na uendeshaji wa Skuli za Binafsi za Maandalizi na Msingi .
Katika kikao hicho Wajumbe hao kwa pamoja wameipitisha Bajeti ya matumizi ya Wizara ya Elimu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.