Taasisi ya Maisha Bora Foundation wametiliana Saini na Jumuiya ya Jamii na Watoto Wajamama kwa lengo la kutekeleza Majukumu ya pamoja ikiwemo kuwaongezea hifadhi kina Mama na Wasichana wanapokuwa katika ada zao za Mwezi
Afisa Mtendaji Mkuu wa Zanzibar Maisha Bora Foundation Ndg.Fatma Fungo amesema wameamua kushirikiana kwa pomoja ili kuhakikisha Wanawake na Watoto wanaimarisha Afya zao
Mtaalamu wa Afya kutoka Kituo cha Afya Mbweni Nafisa Jidawi amesema wanakusudia kuwafikia Wanawake wengi katika kuwapatia Elimu ya Afya,masuala ya lishe ili kuondoa matatizo ya Kiafya katika Jamii
Makubaliano hayo ni sehemu ya kuelekea Siku ya Heidhi salama Duniani ambayo huadhimishwa Duniani kote kila ifikapo Mei 28
stories
standard