Mamlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar, imewataka Wananchi kuimarisha usafi wa mazingira kwa lengo kuiweka haiba nzuri ya Mji sambamba na kukuza Utalii Nchini.
Mkurugenzi Idara ya Elimu Tafiti na Uwekezaji Mamlaka ya Mji Mkongwe, Ndg.Asha Ali Hassan ametoa wito huo wakati wa harakati wa usambazaji wa Vifaa vya kuhifadhia taka huko Malindi amesema Mji Mkongwe ni kivutio kikubwa cha Watalii ambao kwa asilimia kubwa unachangia kukuza pato la nchi kupitia sekta ya utalii.
Amesema mingoni mwa Mikakati iliyopo ni kurekebisha kanuni za usafi kwa kuweka vipengele vya kutoa faini ya papo kwa papo kwa lengo la kuimarisha usafi katika maeneo hayo
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe,Ndg.Ali Said Bakari, amesema utoaji wa Vifaa hivyo vinavyotumia Umeme vimelenga kuimarisha usafi na kuondokana na uchafuzi wa mzingira
Meneja Mkuu Kampuni ya SKY Cleaning Amarido Bashir na Meneja Msimamizi usafi wa Mji Mkongwe, ameiyomba Serikali kuweka kanuni za kutoa adhabu kwa Wananchi wasiotii sheria hasa ya kutupa Taka ovyo katika Maeneo yasiyo rasmi
Baadhi ya Wananchi wa Maeneo hayo wamesema uhifadhi wa mazingira unaepusha Maradhi ya Mripuko yanayoweza kuleta athari katika Jamii
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Vifaa vya kuhifadhia Taka 100, na Gari 16 aina Guta na Pikipiki zinazotumia Umeme