SERIKALI KUENDELEA KUTHAMINI MCHANGO WA ASASI ZA KIRAIA

WAZIRI SAADA MKUYA

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Dkt. Saada Mkuya Salum, amesema Serikali inathamini mchango wa Asasi za Kiraia kama ni Wadau Wakuu wa shughuli za Maendeleo Nchini.

    Akifungua Mafunzo kwa Wadau wa Asasi za Kiraia kupitia mradi wa Uraia wetu huko Mazizini, amesema kupitia juhudi zao wamekuwa wakiunganisha Jamii kwa kuwafikia Wananchi kwa kiasi, kupitia shughuli muhimu ambazo Serikali iliwajibika kufanya hivyo.

    Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar Juwauza Salma Haji Saadat, amesema uendeshaji wao umekuwa ukitegemea zaidi Wafadhili  na wanapokosa hushindwa kuwafikia Wananchi, hivyo ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kushirikiana nao katika  kuwawezesha. 

    Msimamizi wa Mradi wa Uraia wetu Suleiman Baitani ameomba Serikali kulifanyia kazi suala la kuwa na Mwakilishi wa Asasi katika vyombo vya Maamuzi na kushauri kutengenezwa mfumo wa kufanya kazi kwa pamoja na Serikali ili kueleza vikwazo vinavyokabili katika kufanya kazi zao.

   Akitoa Mada katika Mafunzo hayo Wakili Clarence Kipobota, amesema ili  Asasi za Kiraia ziweze kufanya kazi vizuri na Jamii inapaswa kujitathmini wenyewe kwani imebainika kuwa Asasi nyingi zimesahau wajibu wao.

   Mafunzo hayo ya Siku Tatu yaliyoratibiwa na Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar Juwauza na  kufadhiliwa na Foundation for Civil Society yameshirikisha Watendaji wa Asasi mbali mbali za Unguja na Pemba.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.