Akifungua Mafunzo kwa Wadau wa Asasi za Kiraia kupitia mradi wa Uraia wetu huko Mazizini, amesema kupitia juhudi zao wamekuwa wakiunganisha Jamii kwa kuwafikia Wananchi kwa kiasi, kupitia shughuli muhimu ambazo Serikali iliwajibika kufanya hivyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar Juwauza Salma Haji Saadat, amesema uendeshaji wao umekuwa ukitegemea zaidi Wafadhili na wanapokosa hushindwa kuwafikia Wananchi, hivyo ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kushirikiana nao katika kuwawezesha.
Msimamizi wa Mradi wa Uraia wetu Suleiman Baitani ameomba Serikali kulifanyia kazi suala la kuwa na Mwakilishi wa Asasi katika vyombo vya Maamuzi na kushauri kutengenezwa mfumo wa kufanya kazi kwa pamoja na Serikali ili kueleza vikwazo vinavyokabili katika kufanya kazi zao.
Akitoa Mada katika Mafunzo hayo Wakili Clarence Kipobota, amesema ili Asasi za Kiraia ziweze kufanya kazi vizuri na Jamii inapaswa kujitathmini wenyewe kwani imebainika kuwa Asasi nyingi zimesahau wajibu wao.
Mafunzo hayo ya Siku Tatu yaliyoratibiwa na Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar Juwauza na kufadhiliwa na Foundation for Civil Society yameshirikisha Watendaji wa Asasi mbali mbali za Unguja na Pemba.